Waliombaka msichana na kumrekodi video Morogoro sheria itawakaba vipi?

Waliombaka msichana na kumrekodi video Morogoro sheria itawakaba vipi?
Polisi Morogoro walithibitisha kutokea kwa tukio la Mwanamke kubakwa na Wanaume wawili ambao walimrekodi video wakati wakimbaka alafu zikasambazwa mitandaoni. Wameshakamatwa watuhumiwa 11 ambapo tisa kati yao ni kwa kosa la kusambaza picha za utupu huku vijana wawili ambao ni Zuberi Thabiti (30) na Iddy Adamu (32) ni kwa kosa la kufanya mapenzi na msichana huyo kwa nguvu huku wakirekodi. Watuhumiwa walifanya hivyo April 28 2016 saa moja usiku kwenye nyumba ya kulala wageni Dakawa, Mwanamke huyo aliitwa kwenye nyumba hiyo ya wageni na Thabiti ambaye ni mkazi wa Mbarali wilaya ya Mbeya ambaye alikuwa na uhusiano naye kimapenzi. Baada ya kuingia chumbani alimkuta Mwanaume mwingine pia ambapo kwa pamoja walimlazimisha kufanya mapenzi huku mmoja akimrekodi picha za video na baadaye kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Watch Video